Mokiwa Chedy Dominic

Think big, act simple. Happiness is hidden in simple things

About

Our mission is to help people discover the hidden treasure in doing small acts of kindness. Health is capital, and health is built by considering the smallest things. Think big, act simple. Happiness is hidden in simple things.

Mkristo Na Usimamizi Wa Fedha

Mungu wetu ni mwenye upendo mkubwa sana kwa watu wake,

Kabla hajamuumba Mwanadamu alijua kuwa kabisa Mwanadamu huyu anatakiwa kupata mahala pa kufikia pamoja na Rasilimali ambazo zitamsaidia kumudu maisha ya kila siku.

Katika Kitabu cha Mwanzo 1, kinaeleza Uumbaji wa Mungu kwa muda wa siku sita, na Uumbaji huu wa Ulimwengu hauzi na Mwanadamu ila Unaanza na Mazingira ambayo yatamfanya mwanadamu huyu kujisikia vizuri zaidi,

Mungu anakamirisha Uumbaji kwa kumuumba Mwanadamu na kumpa kama mmiriki na mtawala wa kile alichokiumba yaan kwa lugha nyepesi kupitia hivyo ajipatie kula na mahitaji yote ya msingi kama mwanadamu.

Mungu anampa nafasi ya upendeleo hio mwanadamu ya kuwa wakili wa mali ya yake yote. Yaan kwa lugha nyepesi asimamie na kuleta hesabu ya vyote alivyokabidhiwa,

katika makala hii natamani kushare na wewe kanuni chache ambazo zinamfanya mkristo kuwa msimamizi mzuri wa fedha.

Zingatia hili, Kila mmoja anao uwezo wa kutafuta pesa na akazipata ila sio kila mmoja anao uwezo wa kuzisimamia pesa hizo.

Lengo la kupata pesa ni ili tukidhi mahitaji yetu ya msingi lakini kunufaika zaidia na pesa hizo, lakini imekuwa tofauti kwa wengi wetu kunufaika na pesa hizo kwani tumejikuta hatufanyi chochote kile katika eneo la kuizalisha pesa hio, hii ni kwa sababu wengi wetu tunajua kutafuta pesa ila hatujui kuisimamia pesa hio ndio maana imekuwa rahisi kupotea katika mikono yetu.

Twende pamoja katika kanuni hizi ambazo kwazo zitakusaidia kuwa msimamizi mzuri wa fedha zako kila ziingiapo katika mikono yako:

  • 01. Pesa ni za Mungu sio za kwetu

Kwa Mujibu wa Zaburi 24:1 tunakumbushwa kuwa Nchi na Vyote viijazavyo ni mali ya Bwana Dunia na wote wakaao ndani yake, Ikiwemo na Pesa,

Kama hatutagundua kuwa Mungu ndie mmiliki basi pesa nyingi zitakuwa zikipotea bila kujua kwa sababu kanuni zote za usimamizi wa fedha zatoka kwake.

  • 02. Budget

Budget ni moja ya kanuni muhimu katika kuhakikisha mwanadamu anafanya vizuri katika usimamizi wa fedha alizonazo, Wengi wamejikuta wanapotez pesa nyingi kwa kuingia katika matumizi yasiyo ya lazima na wala umuhimu hivo kujikuta wanatumia zaidi ya kile wanachopata na kujikuta hakuna chochote kinachosalia katika mikono yao,

Bajeti ni nguzo muhimu katika usimamzi wa kifedha kwani inanisaidia kujua pesa yangu wapi inatumika na kwa muda gani na kwa nini.

Bajeti inanifanya kuwa na mipaka katika kudhibit pesa isipotee. Kwa maana hio utajikuta wengi wanapoteza pesa zao bila kujua kwa sabbu ya matumzii yasiyokuwa ya lazima.

-Tunapozungumza matumizi elewa sentesi hizi mbili kuwa k:-

a. Kuna matumizi muhimu lkn ni ya lazima

b. Lakini pia kuna matumizi ya lazima lakini sio muhimu kiasi kwamba yakiwepo au yasipokuwepo hakuna madhara yanaweza tokea.

-Anza leo kubana matumizi yako kwa kutengeneza bajeti ya matumizi yako ya siku, wiki na hata mwezi.

-Rekodi kwenye daftari lako la kumbukumbu kila unapofanya manunuzi

-Jifunze kununua vitu kwa bei za jumla hii itakusaidia kuwa na usimamizi mzuri wa pesa upande wa matumizi,

NB: Usifanye matumizi yanayozidi kiwango cha pesa unachoiingiza na kulingana na kiwango cha pesa unachoiingiza kila siku au kwa mwezi.

  • 03: Akiba

Moja ya jambo muhimu sana linalokufanya uwe msimamizi mzuri wa pesa zako ni pamoja na kuweka akiba,

-Suleiman anatumbusha kisa cha mchwa , mdudu mdogo amabe anaakili kubwa nyakati fulani kuwazidi hata wanadamu, Mchwa ni mdudu amabae anajua kusoma nyakati ndio maana kujiwekea akiba kwake ni jambo la kawaida kwa ajili ya nyakati ngumu zinazokuja.

-Hakuna anaejua lini ataingia katika matatizo lkn matatizo huja muda wowote na hayana kubisha hodi, hivo ni salama kujenga tabia ya kuweka akiba kwa nyakati zijazo.

-Niliwahi muuliza mtu mmoja kwa jinsi gani anaelewa kuhusu akiba, Kiukwel Majibu yake yalinishtua sana maana nakumbuka alinambia Akiba ni vitu anavyonunua kama vile TV, Samani za ndani ili siku akipata shida atauza kisha atatue shida yake,

Bila shaka wapo wengi ambao wanajua kuwa vitu hivyo ndio akiba lakini ukweli ni kwamba leo nakwambia Samani za ndani, Nyumba au magari na vingine vingi hivyo sio Akiba.

-Akiba ni pesa inayotunzwa kwa ajili ya kutatua matatizo yanayoweza jitokeza au yatakayojitokeza katika nyakati tusizotarajia hapo baadae,

-Akiba inaweza gawanywa katika maeneo makuu mawili kama ifuatavyo

01. Akiba kama Uwekazaji

02. Akiba kama Dharura.

-Tuanze na Akiba kama Uwekezaji:

Tunalazimika kuweka akiba kwa ajili ya uwekezaji na kupanua wigo wa uchumi wetu zaidi ama kujiongezea vyanzo vya mapato kwa kufanya uwekezaji utakaotupa matokeo chanya.

-Akiba inaweza kuwa njia nzuri kwa mtu anaetaka kuanza biashara anashauriwa kutunza pesa kidogo kidogo kwa ajili ya kuanzisha biashara au kupanua biashara aliyonayo kwanza (Usianzishe biashara kwa pesa za mikopo utalia)

*Unaweza jiuliza nawezaje weka akiba? zipo njia nyingi za kuweza kutunza akiba ni pmoja na kufungua account ya akiba au katika vikoba n.k

Akiba kama Dharura- kama nilivoeleza kuhusu majanga na matatizo yanayoweza kutokea muda wowowte ambayo ukweli ni kwamba akiba ndio itatumika kutatua matatizo hayo na siyo kuuza samani za ndani kutatua matatizo yako, ndio maana unashauriwa kuwekeza zaidi kwenye Asset na Sio Liabilities (Nitafafanua zaidi katika somo lijalo) Dharura hii itunzwe huenda kwa muda wa miezi mitatu mpaka mwaka,

-Jenga mazoea ya kuweka akiba kwa mustakabali wa kesho yako….

Itaendelea………….

imeandikwa na Brayson Kuy

Youth Coach&Creative Designer

Contact: 0758673938/0718258081


Discover more from Holistic Health and Nutrition

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply

Discover more from Holistic Health and Nutrition

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Discover more from Holistic Health and Nutrition

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading