Chakula cha Mtoto Mchanga wa Miezi Sita
Kama tuliyoona katika somo lililotangulia, Shirika la UNICEF linashauri kuwa watoto wachanga wanapaswa kunyonyeshwa kama wanavyohitaji. Yaani mara kwa mara kulingana na wanavyojisikia mtoto anavyojisikia. Kuanzia umri wa miezi 6, watoto wanapaswa kuanza kula vyakula salama. Wanapaswa kula kiasi cha kutosha cha vyakula vya ziada huku wakiendela kunyonya hadi umri wa miaka miwili au zaidi.

Chini ya nusu ya watoto wachanga walio chini ya umri wa miezi 6 wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee. Hii ni kinyume na mapendekezo ya WHO. Hii ni licha ya ukweli kwamba kunyonyesha ni muhimu kwa afya na maisha ya mtoto. Mbali na kutoa nishati na virutubisho katika miezi michache ya kwanza ya maisha, maziwa ya mama ni salama. Pia ni safi katika kuimarisha kinga ya mwili. Pia hupunguza nafasi ya kupata magonjwa kama kisukari, saratani ya matiti na ovari, na inaboresha akili.
Mtoto anapofikisha miezi sita, inashauriwa aanze kupewa vyakula vya nyongeza kilichoandaliwa katika hali ya usafi sana. Watoto hawana budi kula vyakula mchanganyiko kutoka makundi yote 6 ya chakula kwa kiasi cha kutosha. Wape watoto vyakula vyenye madini ya chuma kwa wingi kama vile
- Samaki aliyepikwa na kupondwapondwa,
- Nyama kama vile nyama ya kuku, maini,
- Vyakula jamii ya mikunde na unga ulioongezewa virutubisho vya madini ya chuma ili kuzuia upungufu wa damu mwilini. Unga kama vile mahindi ya njano, Kama vile ambao ni tatizo kubwa kwa watoto wadogo katika nchi zinazoendelea.
- Vyakula ambavyo vina vitamin A kwa wingi ni pamoja na matunda yenye rangi ya chungwa. Matunda kama maembe na mapapai yana rangi ya njano. Pia, mboga za majani kama karoti na nyanya zina vitamin A.
- Mpe mtoto vyakula jamii ya mizizi kama vile viazi vitamu vyenye rangi ya chungwa au njano. Upungufu
- Vyakula kama vile zabibu nzima, karoti mbichi au karanga, vinaweza kusababisha kupaliwa. Watoto ambao bado wanajifunza kutafuna wasipewe vyakula hivyo.
- Nawa mikono kabla ya kumlisha mtoto.
- Inashauriwa pia afundishwe kuombea au kubariki chakula kulingana na imani ya mtoto. Chakula ni ibada.
- Mpe mtoto chakula chenya joto la wastani. Kisiwe cha moto kuepuka kumuunguza mtoto wala kisiwe cha baridi kuepuka kumuumiza mtoto tumbo.
Ni vizuri kuanza kwa kuwapa watoto vyakula laini viilivyoandaliwa kwa usafi sana. Andaa chakula kigumu kidogo kisicho cha majimaji kadri mtoto anavyozidi kuongezeka umri na kukua. Watoto wachanga chini ya umri wa miezi 12 wasipewe maziwa ya ng’ombe. Haishauriwi kuongeza asali, sukari au chumvi kwenye chakula cha nyongeza cha mtoto. Asali humeng’enywa na kusharabiwa taratibu sana katika utumbo. Hivyo huweza kusababisha mtoto kuharisha.

Anza kumlisha mtoto kiasi kidogo cha chakula, ongeza kidogo kidogo kadiri mtoto anavyoongezeka umri. Walezi hawana budi kuwa karibu na mtoto. Ni muhimu mama mzazi au mtu mzima mwenye uelewa na malezi ya watoto akawa ndiye mwangalizi wa mtoto. Usiwaachie watoto kulea mtoto katika umri huu wa miezi sita hadi kumi na mbili. Zingatia ishara zao za mtoto zinazoashiria njaa, uchovu, usingizi au maumivu yasababishayo kukosa utulivu.
Walezi hawana budi kuwalisha watoto polepole na kwa uvumilivu, wakati wa kumlisha mtoto chakula. Mlishe mtoto kwa moyo wa upendo si kwa kumfokea au kumpiga wala kumlaziimisha. Inapendekezwa pia kwamba mlezi azungumze na kumwangalia mtoto usoni mara kwa mara wakati wa kula. Mtoto ni binadamu, japo hajui kuongea hii haimaanishi hawezi kuwasiliana. Anazo lugha za ishara ni budi kuzielewa.

Mazoea Mabaya ya Kuwalisha Watoto
Mazoea yakuwalisha watoto chakula kisichotosha na kisichokidhi mahitaji ya lishe mwilini yanachangia kwa kiasi kikubwa watoto kudumaa. Ni jambo la kawaida katika nchi nyingi kuwaanzishia watoto
wadogo chakula cha nyongeza kabla hawajafi kisha umri wa miezi 6. Sababu zinazotolewa na walezi ni pamoja na
- Kumfanya mtoto mchanga asilie mara kwa mara. Walezi wanachukua hili kama ni dalili ya njaa. Pia wanaamini kwamba mtoto hatosheki na maziwa ya mama pekee.
- Mtoto kulialia ni dalili ya njaa au ni dalili kwamba mtoto hatosheki na maziwa kutoka kwa mama. Dhana hii potofu, zipo sababu nyingine za mtoto kulia mara kwa mara kama vile: kuuchoka, tumbo kujaa gesi. Kumbuka kwamba maziwa ya mama ni chakula tosha kwa mtoto hasa aliye chini ya miezi kuanzia sita. Anapofika miezi sita kuendelea anapaswa kuongezewa chakula cha ziada kwani maziwa pekee hayattatosheleza mahitaji ya mwili.
Hitimisho
Kunyonyesha ni muhimu kwa afya na maisha ya watoto wachanga walio chini ya miezi sita. Ni muhimu kuwapa vyakula vyenye madini ya chuma kadri wanavyokua. Zaidi ya hayo, kujumuisha desturi za kitamaduni kama vile kubariki chakula kunaweza kuongeza uzoefu wa kulisha watoto.


Leave a Reply