Mokiwa Chedy Dominic

Think big, act simple. Happiness is hidden in simple things

About

Our mission is to help people discover the hidden treasure in doing small acts of kindness. Health is capital, and health is built by considering the smallest things. Think big, act simple. Happiness is hidden in simple things.

Namna Bora ya Kuandaa Vyakula: Mwongozo wa Lishe

Vyakula viko katika makundi makuu matatu: Vyakula vya wanga, protini na mafuta. Kazi kubwa haiko sana katika kuvipata vyakula hivi. Bali kazi iko katika kujua namna ya kuandaa vyakula hivyo. Umuhimu na uandaaji wa vyakula hivi hutofautiana. Vyakula hivi vina virutubisho ambavyo huathiriwa sana na maandalizi yake kwa matumizi. Kama vyakula hivi havitaandaliwa kwa makini huharibika hivyo kutofaa tena kwa mahitaji ya mwili.

Mpishi hana budi kujua jinsi ya kuchagua na kuandaa  chakula cha kawaida sana. Chakula  kisicho na viungo vingi ila kinachovutia kwa mlaji na pia kujua ni wakati gani ale chakula gani. Ni jambo la kuzingatia sana kwamba chakula ni sanaa. Chakula huhitaji ubunifu mkubwa katika kuchagua na kukiandaa ili kiwe na mvuto kwa mlaji. Ubunifu ni muhimu sana katika sanaa ya lishe.

Vyakula mbalimbali vya wanga au nafaka huiva kutofautiana sana. Ni muhimu kuvipika kwa muda ili viive vizuri.

Maandalizi Ya Vyakula Kwa Kutegemea Utofauti Wa Aina Zake

Maandalizi ya chakula cha nafaka: UNGA

Kuna mifano mingi ya vyakula vinavyoandaliwa kwa unga kama vile ugali na mikate. Mikate mingi huandaliwa kwa unga wa ngano unga ambao una “glutein”. Gluten ni aina Fulani yap rotini inayosababisha ngano iwe na tabia ya kuvutika.

Utumiaji wa unga uliokobolewa si vizuri kiafya kwa maana hukosa virutubisho muhimu . virutubisho hivyo hubaki kwenye maganda au maganda yake ya nje pale nafaka inapokobolewa. Miongoni mwa matatizo ya kiafya ni pamoja na haja ngumu. Hali hii hutokea hasa anapokosa matunda na mboga za majani katika mlo wake. Tatizo la haja ngumu (au kwa kiingereza constipation) lisipopatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu hupelekea mtu kupata tatizo la BAWASIRI. Haja ngumu pia usababisha kutokwa na damu wakati wa haja (Haemorrhage).

Unga wa nafaka nzima (ambayo haijakobolewa) una vinyuzi vidogo vinavyosaidia katika: Unyonywaji wa majimaji yenye virutubisho katika utumbo. Pia hulinda kuta laini za tumbo na utumbo dhidi ya kemikali za tumboni zinazoweza kuunguza au kumeng’enya ukuta wa tumbo.

Unga wa nafaka isiyokobolewa huwa na nyuzi nyuzi au makapi yanazosaidia umeng’enyaji na usharabiwaji wa chakula katika mfumo wa chakula.

Endapo kuta zitaathiriwa na kemiikali za tumboni, hupelekea vidonda pamoja na maumivu ya tumbo. Kadharika nyuzi nyuzi husaidia wadudu wa tumboni kupata nafasi ya kujishikiza hivyo kurahisisha shughuli yao ya kumeng’enya chakula tumboni.

Ni sababu hizo ndizo zinazotutaka kuwa na umakini katika uandaaji wa vyakula jamii ya nafaka. Zingatia mambo yafuatayo unapoandaa chakula cha nafaka.

  • Usikoboe nafaka zinazofunikwa na ngozi laini kama vile mahindi, mtama, uwele, ulezi na jamii zake. Ni vizuri kuziotesha kidogo kabla ya kusaga endapo unahitaji kutumia unga wake kwa ajili ya uji. Chambua na uoshe vizuri, kisha zitandaze mahali safi. Ndani ya siku tatu zitaanza kuota. Zianike na kiisha kusaga kwa matumizi ya unga wa uji au ugali. Sababu ya kufanya hivi ni kuwa, mbegu hutunza sukari ngumu. Pia, huifadhi virutubisho vingine ili kujiandaa na msimu wa kuchipuka. Mbegu inapokuwa haijasisimuliwa kuota, virutubisho hivyo hufichwa katika hali ambayo ni ngumu kwa mwili kuvipata. Mbegu inayoanza kumea kuwa na wingi wa madini ya magnesium, phosphorus na vitamin K na amino acids.
  • Kwa kuwa mbegu hutunza sukari tata (complex sugar) kwa ajili ya kimea, basi ni vizuri kuchemsha unga kwa muda mrefu. Hii inasaidia kuivunjavunja sukari iwe katika hali ya sukari nyepesi. Chemsha uji wa kunywa au pika ugali kwa muda wa kutosha. Kutokufanya hivyo hupelekea kuharisha.

Uandaaji wa Maziwa

Maziwa ni chakula kamili kwa watoto wa wanyama katika kundi la mamalia. Tunasema ni chakula kamili kwa sababu kina virutubisho vyote kwa ajili ya mtoto anayenyonya. Makundi yote ya vyakula ikiwemo wanga au sukari, mafuta, protini pamoja na madini na vitamini hupatikana katika maziwa.

Maziwa yanapoandaliwa vizuri kwa nia ya kutoharibu virutubisho vilivyoo ndani yake, basi huleta matokeo chanay akwa mtumiaji. Ziko njia mbalimbali zinazotumika kuandaa mazziwa ikiwemo ikiwemo kuyachemsha. Mbinu nii ni maarufu sana miongoni mwa watumiji wengi wa maziwa. Bai unapoyachemsha hakikisha unayachemsha kwa muda mfupi ili kuua vijududu vya maradhi tu kwa maana kuna vijidudu rafiki ambavyo huhitajika mwilini. Usichemshe maziwa kwa moto mwingi ndani yamuda mfupi, bali kwa moto mdogo kwa muda mrefu. Njia hii huitwa pasteurization.

Chemsha maziwa kwa moto mdogo na kwa muda mrefu kama wa dakika 15-30. Mbinu hii itasaidia kudumisha bakteria rafiki kama vile Lactobacillus. Pia, inasaidia kupunguza kiwango cha maji katika maziwa kwa njia ya mvuke.

Maziwa ni kimiminika chenye protini nyingi. Protini inapopitishwa kwenye moto mkali kwa mufa mfupi au mrefu, huharibika. Kitendo cha protini kuharibika huitwa protein denaturation. Maziwa pia yana sukari ya asili inayoitwa Lactose. Hivyo haipaswi kuongeza sukari nyingine katika maziwa.

Kumbuka protini hutofautiana. Kwa mfano protini iliyoko katika maziwa ni tofauti na iliyoko katika maharage hivyo uandaaji wake pia ni tofauti. Pika maharage na mboga nyingine jamii hii mpaka yaive vizuri na kulainika.

Uandaaji wa Mboga za Majani

Mboga za majani zina vitamin na madini kwa wingi sana. Vitu hivi huweza kuharibika kirahisi wakati wa uandaaji. Pia radha na ugumu wa mboga huathiriwa zaidi na jinsi inavyopikwa. Ili kuandaa mboga za majani katika hali ya kudumisha afya yake basi

  • Hakikisha unazichambua na kuziosha kwa makini.
  • Tumia maji safi yanayotiririka au tumbukiza katika vyombo tofauti vyenye maji safi.
  • Osha kama unavyosuuza vyombo au nguo. Hii itakusaidia kuondoa uchafu wote wa shambani pamoja na wadudu.
  • Usiloweke mboga hasa baada ya kuzikata kata. Kama tulivyosema katika somo lililopita, mboga za majani huwa na vitamini zinazoharibika katika maji. Vitamini kama vile C, B, G huyeyuka na kupotea unapoosha mboga au kuziloweka zikiwa zimeshakatwa katwa.
  • Unapochambua mboga, usiondoe nyuzinyuzi zake na kutupa
  • Mboga za majani zisikae muda mrefu motoni, Zipike kwa dakika tano mpaka kumi. Pika kuua vijidudu vya maradhi na si kuua mboga. Hakikisha unadumisha ukijani na ugumu wa mboga. Kumbuka si mboga zote utapaswa kuzipika kwa dakika tano mpaka kumi, unachopaswa kufanya ni kuzingatia usafi na usalama wa unakozitoa. Pia kuna mboga za majani magumu kama kisamvu, ni vizuri ukakipika kwa muda mrefu mpaka kiive vizuri.

ZINGATIA: Matumizi ya vyakula asilia ambavyo havijapikwa au vilivyopikwa kwa muda mfupi yanasaidia mwili kupambana na magonjwa. Vyakula hivi vinapatia mwili virutubisho vilivyo hai vinavyoimarisha kinga ya Mwili.

Vyakula vya asili visivyopikwa au vilivyopikwa kidogo ni vizuri kwa afya ya mwili. Huupunguzia mwili mzigo wa umeng’enyaji na pia huupa mwili virutubisho na vimeng’enya (enzymes) hai.

Bonyeza link hiyo kwa somo lililopita


Discover more from Holistic Health and Nutrition

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply

Discover more from Holistic Health and Nutrition

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Discover more from Holistic Health and Nutrition

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading